Kambi ya mafunzo kwa Vijana yamalizika jijini Dar

Kwaya ya Gracias kutoka Korea ikitumbuiza katika kambi ya Vijana iliyomalizika jana katika viwanja vya mikutano vya Mlimani City.Kambi iyo mwaka huu imefanyika nchini ikijumuisha vijana elfu tatu duniani kote.
Mkurugenzi msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Bi. Esther Riwa akiongea na Vijana mbalimbali baada ya Kuwapa somo kuhusu kuwa na Fikra Chanya ili kujiletea maendeleo na Stadi za Maisha.Vijana hao wameweka kambi katika Viwanja vya mikutano vya mlimani city jijini Dar es Salaam wakijifunza mambo mbalimbali.
Naibu katibu mkuu kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Elisante Ole Gabriel akizungumza na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Vijana Duniani Bw Ock Soo Park katika Viwanja vya Mlimani city alipokuwa akifunga kambi ya Vijana yenye kauli mbiu Badilisha Fikra iliyoshirikisha vijana elfu tatu kutoka duniani kote.
Naibu katibu mkuu kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akiwa katika majadiliano na viongozi wa mbalimbali wa Taasisi ya kimataifa ya Vijana Duniani,Kushoto kwake ni Mwanzilishi wa Taasisi iyo Bw Ock Soo Park na kulia kwake ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya maendeleo ya Vijana kutoka Wizara iyo Bi Esther Riwa.
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.