ARSENE WENGER AJIBU MATAMSHI YA GARY NEVILLE KUHUSU 'KIBURI' CHAKE

Arsene Wenger Kocha wa ArsenalArsene Wenger amesema kuwa Gary Neville hakuwa sahihi kudai kwamba meneja huyo wa Arsenal “hajui au ni mwenye kiburi” kwa kutokifanyia marekebisho kikosi chake kuendana na washindani wake wa Ligi Kuu.

Kabla ya sare tasa na Liverpool jana Jumatatu, Neville alisema kwenye kipindi cha televisheni kuwa Arsenal ilihitaji kusajili wachezaji wapya wenye “uwezo” ili kuwapa nguvu zaidi wachezaji wenye vipaji Washika bunduki hao, na kusema kuwa kiburi pekee ndicho kinachomfanya Wenger asitumie mbinu mpya.

Alipoulizwa kuhusu kauli za Neville baada ya mchezo huo, Wenger alisema: "Kila mtu ana mawazo yake. Ninaweza kukuthibitishia kuwa hilo sio lazima liwe sahihi.”

Neville alikuwa akizungumzia tabu anayoipata Francis Coquelin na Santi Cazorla wanapocheza nafasi ya kiungo kabla ya kufanya mabadiliko hafifu ya Calum Chambers na Gabriel.
"Kwangu mimi ni kiburi. Naamini ni kiburi. Hivyo ndivyo ninavyoamini,” alisema Neville. Kudhani kwamba hutaifanyia marekebisho timu yako kuendana na nguvu za timu unazocheza nazo.

"Ama hajui, au ni kiburi. Kwa sababu wanaendelea kupoteza michezo namna hii. Nadhani ni kosa.

"Nina heshima kubwa kwa Arsenal kama klabu. Kazi ya Arsene Wenger ni nzuri sana.

"Lakini sioni kwa nini hasajili wachezaji wapya kusaidiana na wachezaji hawa wenye vipaji ulio nao ili kuwawezesha kushinda ligi.

"Ni tatizo kubwa kwa Arsene Wenger kwa miaka hii 10 ukiangalia kwa nini hajagundua tatizo kwa aina hii ya wachezaji [kama vile Coquelin na Cazorla] – kwa sababu hawawezi kushinda ligi wakiwa nao. Haiwezi kutokea.

"Sina neno muafaka linaloweza kuwaelezea. Ninaweza kufanya hivyo, lakini haitakuwa na manufaa kulizungumza kwenye televisheni.

"Wao si wachezaji wanaweza kukufanya ushinde ligi… unahitaji wachezaji imara, wenye nguvu unazozihitaji kwenye timu kuweza kukabiliana na timu nyingine ikiwa  Blackburn au Manchester City yenye wachezaji imara kama Yaya Toure na  Vincent Kompany."
Wenger aliyakosoa vikali matamshi hayo baada ya timu yake kuweza kutoa sare ya kutofungana na Liverpool.

"Utapata aina zote za sifa kwangu tangu nilipofika hapa,” Wenger alisema. “Nimefanya kazi yangu vizuri kwa miaka 20. Ninawaachia wengine watoe tathmini ya kiwango cha kazi yangu.

"Unapokuwa hujashinda unachukuliwa vibaya na watu hupata sababu za kusema. Je, ni sababu nzuri? Nina uzoefu wa kutosha kujua ni wakati gani muafaka na upi ambao sio muafaka.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.