BAN KI-MOON AMFUTA KAZI MKUU WA JESHI LA KULINDA AMANI

UN Secretary-General Ban Ki-moon (© AFP)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-MoonKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemfuta kazi mkuu wa Ujumbe wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya skendo nyingine ya udhalilishaji wa kingono kuvikumba vikosi vya ulinzi wa amani nchini humo.

Ban amesema kuwa amemtaka Babacar Gaye kuachia ngazi, na kwamba mwanadiplomasia huyo kutoka Senegal amewasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Hatua hiyo imekuja baada ya shirika la Amnesty International kumtuhumu askari mmoja wa kulinda amani kuwa alimbaka binti wa miaka 12. Aidha, vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa vilimpiga risasi na kumuua kijana mmoja pamoja na baba yake wakati wa operesheni ya hivi karibuni kumsaka kiongozi wa zamani wa waasi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, limesema shirika hilo.

Jinai hilo iliyofanyika Agosti 2 na 3 ilisababisha pia kuuawa kwa mlinda amani kutoka Cameroon na watu wengine wanne.

Madai kama hayo ya kuwadhalilisha watoto yaliwahi kutolewa dhidi ya askari wengine wa UN nchini humo.

“Umoja wa Mataifa inapopeleka walinda amani, tunafanya hivyo ili kuwalinda watu walio katika hali mbaya kabisa duniani,” alisema Ban na kuongeza, “Sitavumilia kitendo chochote cha watu wanaobadilisha uaminifu kuwa hofu.”

Babacar Gaye, mkuu wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Aidha, kuna tuhuma za dhulma za ngono zinazodaiwa kufanywa na askari wa Ufaransa, huku ripoti mbalimbali zikisema kuwa waliwadhalilisha watoto kingono katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kubadilishana na chakula. Ufaransa inasema kuwa inayafanyia uchunguzi madai hayo.

“Siwezi kuelezea jinsi nilivyofazaishwa, kukasirishwa na kuaibishwa na taarifa za hivi karibuni kuhusu miaka ya dhulma za kingono zilizofanywa na vikosi vya UN… inatosha,” alisema Ban.

Jamhuri ya Afrika ya Kati iliingia katika machafuko tangu Desemba 2013 baada ya makundi ya Kikristo yenye silaha kuanzisha mashambulizi dhidi ya kundi la Seleka lenye Waislamu wengi ambalo liliiangusha serikali mwezi Machi mwaka huo.

Tangu Januari 2014, nchi hiyo imekuwa ikiongozwa na serikali ya mpito. Uchaguzi wa Urais na Ubunge umepangwa kufanyika Oktoba 18.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.