EL HADJI DIOUF AJIPANGA KUWA MWANASIASA

Former Senegal forward El Hadji Diouf in
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal, El Hadji Diouf akiwa dimbani.


Umaarufu wa El Hadji Diouf katika soka na mikiki yake dimbani vinajulikana ulimwenguni, lakini baada ya heshima aliyoitengeneza katika michuano ya Kombe la Dunia na Ligi Kuu ya Uingereza, mkongwe huyo anasaka mafanikio ya kisiasa katika nchi yake ya Senegal.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 34 aliyetengeneza jina lake katika kikosi cha Senegal kilichowaadhiri mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Ufaransa, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo mwaka 2002 nchini Korea Kusini, anakaribia kuachana na soka akiwa na kilabu ya Sabah FC inayocheza daraja la pili nchini Malaysia.

Mafanikio yake katika mchezo wa soka yalimpeleka katika klabu za Sochaux, Rennes na Lens za Ufaransa, kabla ya kuchukuliwa na klabu za Uingereza na Scotland kama vile Liverpool, Bolton, Sunderland, Blackburn, Glasgow Rangers, Doncaster Rovers na Leeds United.

Katika tasnia ya soka hakuna anayebisha kuwa ni mchezaji mzuri na daima hufurahia kuongea na mashabiki wake na wanahabari.

Lakini Diouf pia amekuwa mtu mwenye milipuko ya hasira. Matukio kadhaa ya kuwatemea mate wachezaji wa timu pinzani na mashabiki yaliweka wingu katika mafanikio yake katika soka.

Katika mahojiano ya hivi karibu na shirika la habari la AFP mjini Kuala Lumpur, Diouf alisema kuwa hatua ya timu yake ya taifa kufikia robo fainali katika mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2002 ndio kiwango cha juu alichofikia katika maisha yake ya soka.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.