AL-SHABAB WATWAA MJI MWINGINE

Al-Shabab militants in Somalia (file photo)
Wanamgambo wa Al-Shabab nchini SomaliaKundi la wanamgambo wa al-Shabab limeutwaa mji mwingine katika eneo la katikati mwa Somalia baada ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AMISOM) kuondoka katika eneo hilo.

“Leo tumeuchukua mji wa Buqda kwa amani. Mji huo sasa upo chini ya udhibiti wetu,” msemaji wa kundi hilo, Sheikh Abdiasis Abu Musab, amesema.

Vikosi vya AMISOM, ambavyo viliudhibiti mji huo kutoka kwa wanamgambo hao mwezi mmoja uliopita, viliondoka katika mji huo Jumamosi usiku. Ahmed Nur, afisa mwandamizi wa jeshi la Somalia, amesema kuwa askari wameondoka katika mji huo kwenda kupambana na al-Shabab katika maeneo mengine, na kwamba watarudi.

Huu ni mji wa tatu kuangukia mikononi mwa wanamgambo hao tangu siku ya Ijumaa.

Ndani ya siku tatu zilizopita wanamgambo hao wameitwaa miji ya El Saliindi, kilometa 65 (maili 40) kusini mwa mji mkuu, Mogadishu, na mji wa Kuntuwarey, ulio baina ya Mogadishu na bandari ya Barawe, yote ikiwa katika jimbo la Shabelle ya Chini.

Kundi hilo ambalo linalenga kuiangusha serikali ya Somalia, hufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya maafisa wa serikali na walinda amani wa AMISOM nchini humo.

Mapema Jumamosi, wanamgambo hao waliushambulia msafara wa AMISOM nje ya mji wa Marka na kusababisha vifo.


Somalia imekuwa katika ghasia baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa al-Shabab tangu mwaka 2006.


Mwaka 2011, wanamgambo hao waliondolewa mjini Mogadishu na miji mingine mikubwa nchini humo katika makabiliano yaliyoendeshwa na vikosi vya serikali kwa kushirikiana na vikosi vya AMISOM vinavyoundwa na askari kutoka Uganda, Ethiopia, Burundi, Djibouti, Kenya na Sierra Leone.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.