GUATEMALA YAMZUIA RAIS KUSAFIRI NJE YA NCHI

Guatemalan President Otto Perez (AFP photo)
Rais wa Guatemala Otto PerezRais wa Guatemala amezuiliwa na mahakama kuondoka nchini mwake kufuatia fukuto la kashfa ya ufisadi wa mamilioni ya dola iliyoukumba utawala wake.

Ofisi ya mwendesha mashitaka iliiomba mahakama kumzuia Rais Otto Perez na mahakama ililikubali ombi hilo.

Hukumu hiyo imetolewa saa chache baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura kwa wingi kumuondolea kinga rais huyo na hivyo kumfanya aweze kushitakiwa.

Anatuhumiwa kuhusika na mpango ambao wafanyabiashara wataweza kutoa hongo kukwepa ushuru wa forodha.

Mwendesha mashitaka Thelma Aldana amesema kuwa rais Perez anachunguzwa kutokana na uwezekano mkubwa wa kuhusika na hongo na ukwepaji wa ushuru wa forodha.

"Guatemala inaonesha kuwa hakuna aliye juu ya sheria, na huu ni ujumbe wa watumishi wa umma wa sasa na wa baadaye kwamba mienendo yetu lazima iendane na mamlaka ya katiba”, amesema.

Aidha, msemaji wa Rais amesema kuwa rais huyo anautambua mchezo huo, ambao si mzuri ingawa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kutokea, na kuongeza kuwa ataheshimu utawala wa sheria.


Makamu Rais wa zamani wa nchi hiyo Roxana Baldetti, ambaye msaidizi wake binafsi alitajwa kuongoza kashfa hiyo, na idadi kadhaa ya mawaziri, wameshajiuzulu kutokana na sakata hilo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.