RASMI: MAN UNITED WAMNYAKUA MARTIALManchester United imetangaza kumsajili Anthony Martial kutoka Monaco.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 mwanzo alihusishwa na kuhamia Tottenham kabla ya kusaini mkataba mpya pale Stade Louis II lakini sasa amekuwa mtu wa sita kusajiliwa na Louis van Gaal katika msimu huu wa majira ya joto kwa ada ya paundi milioni 36 (yuro milioni 50).

Baada ya Robin van Persie kujiunga na Fenerbahce mwezi Julai na Javier Hernandez anayetarajiwa kuelekea Bayer Leverkusen, usajili wa straika mpya ilikuwa kipaumbele cha United kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Kwa sasa Wayne Rooney amekuwa na uchezaji usioridhisha katika Ligi Kuu tangu kuhamia Old Trafford mwaka 2004, huku akiwa hajafunga hata bao moja ndani ya michezo 10, tofauti na msimu uliopita ambapo alifanya vyema.


Martial amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu sana katika Ligi ya Ufaransa na inaripotiwa kuwa bosi wa Monaco Leonardo Jardim alikuwa ametishia kuondoka iwapo angeuzwa kwa United.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.