RONALDO AVUNJA REKODI YA UFUNGAJI


Katika mchezo wa kuvutia dhidi ya Espanyol hapo jana, Cristiano Ronaldo alifunga mabao 5 – ikiwa ni pamoja na hat trick – na kuweka rikodi mpya kama mchezaji wa Real Madrid aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga.

Nyota huyo kutoka Ureno ameifungua Real Madrid mabao 230 katika La Liga, mabao mawili zaidi ya Raul Gonzales aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo.

Mshindi huyo wa Ballon d'Or wa mwaka 2015 alitumia michezo 204 kufunga mabao mawili zaidi ya Raul aliyetumikia michezo 550.

Jana Real Madrid iliichachafanya Espanyol 6 – 0 (Benzema 28, Cristiano Ronaldo, 7, 17 (P), 20, 62 na 81) katika mchezo wa ugenini na hivyo kushikilia uongozi wa ligi kwa muda baada ya michezo mitatu.

Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kufunga magoli 5 katika mechi moja, mara ya kwanza ikiwa ni katika mchezo dhidi ya Granada mwezi Aprili (9 – 1).

Orodha ya wafungaji bora katika La Liga inaongozwa na Lionel Messi (286), akifuatiwa na Hugo Sanchez (234), Telmo Zarra (251) na Cristiano Ronaldo.

Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester United kwa kitita cha uhamisho wa yuro milioni 94 kilichovunja rekodi wakati huo.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.