SERIKALI YA MISRI YAJIUZULU

Egyptian Prime Minister Ibrahim Mahlab (AFP)
Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab


Serikali ya Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab imewasilisha barua ya kujiuzulu katika ofisi ya rais wa nchi hiyo.

"Waziri mkuu amekabidhi barua ya kujiuzulu kwa serikali yake kwa rais ambaye ameipokea,” ilisema taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikufafanua zaidi sababu za kujiuzulu kwa serikali hiyo.

Imeripotiwa kuwa Mahlab ameombwa kuhudumu kama waziri mkuu wa mpito mpaka serikali mpya itakapoundwa. Sisi amemtaka waziri wa mafuta, Sharif Ismail, kuunda serikali mpya ndani ya wiki moja.


Aliyekuwa Waziri wa Kilimo wa Misri Salah El Din Mahmoud Hilal

Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya waziri wa kilimo Salah El Din Mahmoud Hilal kujiuzulu na kisha kutiwa nguvuni kwa tuhuma za ufisadi.

Hayo yanatokea wakati watumishi wa sekta ya umma wakipanga kufanya maandamano makubwa kupinga sheria ya utumishi wa umma yenye utata, ambayo hivi karibuni ilipitishwa na Sisi. Waziri wa mambo ya ndani ameapa kuzima maandamano hayo.

Misri ilikumbwa na ghasia tangu kupinduliwa kwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, Mohammed Mursi, katika mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Julai mwaka 2013 yaliyoungwa mkono na Sisi, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo.

Baada ya mapinduzi hayo, maelfu ya wafuasi wa Mursi waliwekwa korokoroni, wengi wao wakihukumiwa adhabu ya kifo akiwemo Mursi mwenyewe.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.