VENEZUELA NA COLOMBIA ZAKUBALINA KUMALIAZA TOFAUTI ZAO

(From L) Foreign ministers of Venezuela, Ecuador, Colombia and Uruguay, Delcy Rodriguez, Ricardo Patino, Maria Angela Holguin and Rodolfo Nin Novoa attend a dialogue session in the Ecuadorian capital, Quito, September 12, 2015. ©Reuters
(Kutoka kushoto) Mawaziri wa Mambo ya nje wa Venezuela, Ecuador, Colombia na Uruguay, Delcy Rodriguez, Ricardo Patino, Maria Angela Holguin na Rodolfo Nin Novoa wakihudhuria mazungumzo katika mji mkuu wa Ecuador, Quito, Septemba 12, 2015.Colombia na Venezuela zimekubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia uliovunjika baada ya mgogoro wa mipaka baina ya mataifa hayo mawili ya Amerika ya Kusini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia Maria Angela Holguin na mwenzake wa Venezuela, Delcy Rodriguez, wamekutana katika mji mkuu wa Ecuador, Quito hapo jana.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ecuador Ricardo Patino na mwenzake wa Uruguay Rodolfo Nin Novoa, ambao serikali zao zimekuwa zikiwataka maafisa wa Bogota na Caracas kumaliza tofauti zao, walihudhuria pia.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyosomwa na Patino, wanadiplomasia hao waandamizi kutoka Colombia na Venezuela walipiga “hatua ya kuridhisha” katika kushughulikia “masuala nyeti”, na watashauriana na viongozi wao kuhusu mipango ya kuwakutanisha marais wao kutatua kukamilifu mgogoro huo wa mipaka.

Mkutano wa awali baina ya Holguin na Rodriguez uliofanyika Agosti 26 haukuzaa matunda.

Raia wa Venezuela wakirudi kutoka Colombia wakiwa wamekwama mpakani katika eneo la Paraguachon katika jimbo la Venezuela la Zulia, Septemba 10, 2015.


Bogota na Caracas zimekuwa katika mgogoro tangu mwezi jana, baada ya Rais wa Venezuela Nicolas Maduro kufung sehemu ya mpaka wa nchi hizo.

Uamuzi huo ulikuja baada ya askari watatu wa Venezuela kushambuliwa na watu wenye silaha wakati wakifanya operesheni dhidi ya magendo katika mji wa San Antonio katika jimbo la Tachira Aprili 19.

Mataifa hayo yaliwaita mabalozi wao kufuatia mzozo huo, jambo lililosababisha kufukuzwa kwa kiasi cha raia 1,500 wa Colombia wanaoishi Venezuela.

Mpaka huo wenye urefu wa kilometa 2,200 (maili 1,400) ni eneo lenye msitu mkubwa ambapo shughuli nyingi za magendo na biashara haramu hufanyika.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.