WINCHI YAANGUKA MSIKITI WA MAKKA, MAHUJAJI KADHAA WAPOTEZA MAISHARipoti zinasema kuwa kwa uchache watu 65 wamepoteza maisha baada ya winchi kuwaangukia Mahujaji katika Msikiti Mkuu wa Makka, Saudi Arabia.

Mamlaka ya nchi hiyo zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kueleza kuwa zaidi ya watu 154 wamejeruhiwa. 

Duru kutoka nchini humo zinasema kuwa upepo mkali ulioandamana na kimbunga ndio uliosababisha kuanguka kwa winchi hiyo.

Mashuhuda wanasema kuwa magari ya wagonjwa yaliwasili katika eneo hilo na kuwaondoa majeruhi.

Miradi kadhaa ya ujenzi imekuwa ikifanyika katika mji wa Makka kwa miaka kadhaa. Miradi hiyo inalenga kuupanua Msikiti Mkuu na maeneo yanayouzunguka.

Tukio hilo linatokea wakati maelfu ya mahujaji wa Kiislamu wakimiminika katika mji huo mtukufu kwa ajili ya ibada ya hijja ambayo hufanyika kila mwaka.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.