ZAIDI YA MAHUJAJI 700 WAPOTEZA MAISHA MJINI MAKKA

A man receives resuscitation after a stampede in Mina near Mecca, Saudi Arabia, September 24, 2015.
Hujaji akipata huduma baada ya ajali ya kukanyagana katika eneo la Mina Septemba 24, 2015

Kwa uchache mahujaji 717 wamepoteza maisha na wengine wapatao 863  wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokana na kukanyagana katika eneo la Mina nje ya mji wa Makka, vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vimeripoti.

Kituo cha televisheni cha al-Ekhbariya kimeripoti maafa hayo kutokana na taarifa za polisi ya nchi hiyo.


Tukio hilo limetokea katika eneo la Mina wakati mahujaji wakishiriki katika tukio la kupiga mawe viguzo ambavyo ni alama ya shetani.

Watu wakiwa wamelala chini baada ya mkanyagano wa mahujaji katika eneo la Mina nje ya mji wa Makka, Saudi Arabia Septemba 24, 2015.

Kiasi cha watu milioni 2 wanashiriki katika ibada ya Hijja mwaka huu mjini Makka.

Hayo yanatokea baada ya tukio la winchi ya ujenzi kuanguka katika Msikiti Mkuu wa Makka na kuua zaidi ya watu 100 huku zaidi ya watu 200 wakijeruhiwa.


Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.