IRAN YAPOTEZA MAKAMANDA WENGINE NCHINI SYRIA

IRGC Brigadier General Farshad Hassounizadeh, who was killed by Daesh Takfiris in Syria on October 12, 2015.
Brigedia Jenerali Farshad Hassounizadeh aliyeuawa Oktoba 12, 2015 nchini Syria.


Majenerani wawili wa Kiiran wameuawa nchini Syria katika mapambano na  wanamgambo wa kundi la Dola ya Kiislamu katika Iraq na Sham (ISIS), ripoti zinasema.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Hamid Mokhtarband na Farshad Hassounizadeh, ambao wote wana cheo cha brigedia jenerali katika jeshi la walinzi wa mapinduzi la nchi hiyo, wameuawa jana Jumatatu.

Brigedia Jenerali Hamid Mokhtarband aliyeuawa nchini Syria mnamo Oktoba 12, 2015

Majerali hao wameuawa siku chache baada ya kuuawa kwa kamanda mwandamizi katika jeshi hilo, Brigedia Jenerali Hossein Hamedani, ambaye aliuawa na wanamgambo hao katika viunga vya mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria.

Iran ilituma askari kumsaidia rais wa nchi ya Syria, Bashar Al-Assad, anayepambana na uasi uliodumu kwa muda wa miaka 4 sasa.

Ghasia nchini humo zilizuka mwezi Machi 2001 na mpaka sasa zaidi ya watu 250,000 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya milioni moja wamejeruhiwa, kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.