ERDOGAN: TATIZO LA UGAIDI LINAHITAJI JUHUDI ZA PAMOJA

Turkey's Erdogan: Terrorism requires global response ANTALYA, Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa mashambulizi ya Ijumaa mjini Paris yameonesha kwamba uchumi na usalama wa dunia ni mambo yenye uhusiano, na kuongeza kuwa masuala ya kiulimwengu kama vile ugaidi, vita vya kiraia nchini Syria na tatizo la wakimbizi ni mambo yanayohitaji juhudi za dunia nzima.


 "Mashambulizi ya kigaidi mjini Paris kwa mara nyingine yameonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa baina ya uchumi na usalama na hatuwezi kuupuuza uhusiano huu wa karibu”, amesema Erdogan wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa duniani (G20) unaofanyika katika mji wa Antalya kusini mwa Uturuki.

Rais huyo amesema kuwa suala la uchumi ndio lengo kuu la G20 lakini jukwaa hilo la kimataifa haliwezi kukwepa jukumu la kushughulikia matatizo ya kisiasa, kijamii au kiutamaduni yanayoisumbua dunia.

"Matukio yote haya yanatuonesha kuwa ugaidi ni tishio kwa amani na usalama wetu sote. Sisi kama Uturuki, tunaamini kwamba ushirikiano imara baina ya mataifa katika kukabiliana na ugaidi ni jambo ambalo tunapaswa kulichukulia azma madhubuti.”

Kuhusu kadhia ya wakimbizi, Erdogan aliashiria wazi kuwa jumuiya ya kimataifa “imeshindwa mtihani huo”.

Erdogan amesema kuwa wakati Uturuki ikikalia kiti cha uongozi wa G20, imefanya maamuzi makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu, nishati na kuongeza fursa za ajira kwa wanawake.


"[G20] sio sio taasisi tutakayoikumbuka kama jukwaa wakati wa matatizo pekee. Bali kuna matarajio mengine ambayo dunia inayatarajia kutoka kwetu. Kwa kulielewa hili, ningependa kusema kuwa uenyekiti wa Uturuki umejikita kwenye ushirikishaji, utekelezaji na uwekezaji. Katika utamaduni na ustaarabu wetu, haya ndio mambo muhimu.”


"Dhana ya haki ni dhana nyeti katika utamaduni wetu. Ninaamini kwamba inaafikiana na ushirikishaji katika majukumu ya G20. Jambo hilo tumelipa umhimu wa karibu. Kipaumbele cha pili ni utekelezaji: hakika tunataka kutekeleza kauli na ahadi zetu. Jambo la tatu ni uwekezaji. Takribani katika mataifa yote yaliyoendelea na yanayoendelea bado kuna hitajio la miundombinu. Kwa muktadha huu wanachama wetu wanatilia maanani vipaumbele hivi kwa ajili ya maslahi ya nchi zao. Wameweka mikakati ya uwekezaji ambayo wataitekeleza,” amesema Erdogan.

Uturuki ni mwenyeji wa mkutano wa 10 viongozi wa mataifa 20 yenye uchumi mkubwa (G20), ambao unajadili matatizo makubwa ya kisiasa na kiusalama duniani ikiwemo suala la Syria na tatizo la wakimbizi.


CHANZO: Anadolu Agency
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.