'PUTIN, MTU MWENYE NGUVU ZAIDI DUNIANI

Russian President Vladimir Putin (AFP)
Rais wa Urusi Vladmir Putin


Rias wa Urusi Vladimir Putin amechaguliwa na jarida la Forbes kwa mara ya tatu kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani.

Putin amempita Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye amekuwa wa tatu baada ya Kansela wa Ugerumani Angela Merkel, aliyechaguliwa kuwa mwanamke mwenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani katika orodha hiyo ya saba inayotolewa kila mwaka na iliyochapishwa jana Jumatano.

"Putin ameendelea kuthibitisha kwamba yeye ni miongoni mwa watu wachache duniani wenye uwezo wa kufanya kile wanachokitaka,” limeandika jarida hilo.

Kwa mujibu wa makala hayo, ushawishi wa Putin ndani ya nchi yake umepanda mpaka asilimia 89, ambacho ni kiwango cha juu zaidi ndani ya miaka sita.

USHAWISHI WA OBAMA UMETIKISIKA

Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani aliyeshindwa kuwa katika mbili bora. "Wakati Obama akiwa katika mwaka wa mwisho wa utawala wake, ni wazi kuwa ushawishi wake umetikisika, na imekuwa ngumu zaidi kufanikisha mambo,” limesema jarida hilo.

Kati ya watu 73 katika orodha hiyo ya mwaka 2015, Papa Francis amekuwa wa nne huku Rais wa China Xi Jinping akishika nafasi ya tano, ambapo ameporomoka kwa nafasi mbili za mwaka jana.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.