UTURUKI YAITUNGUA NDEGE YA URUSI

A file picture taken on October 3, 2015 shows a Russian Sukhoi Su-24 bomber taking off from the Hmeimim airbase in the Syrian province of Latakia. (AFP)
Ndege ya Urusi aina ya Sukhoi Su-24 ikiruka kutoka uwanja wa Humeimim katika mkoa wa Latakia nchini Syria.

Ndege ya kivita ya Urusi imetunguliwa leo na jeshi la anga la Uturuki katika mkoa wa Kızıldağ karibu na mpaka wa Syria.

Ikulu ya Uturuki imethibitisha kuwa ndege hiyi aina ya SU-24 imetunguliwa baada ya kuingia katika anga ya nchi hiyo.

Taarifa iiliyotolewa na jeshi la anga la nchi hiyo imesema kuwa ndege hiyo ilionywa mara 10 ndani ya dakika 5 kabla ya kutunguliwa.

Marubani wawili wameripotiwa kuruka kwa kutumia miamvuli yao. Haijawa wazi iwapo wamepona au la.

Hata hivyo, Urusi imekanusha kuwa ndege yake ilikiuka sheria za anga, na taarifa ya wazara ya ulinzi imeeleza kuwa helkopta za Urusi zinafanya uchunguzi katika eneo hilo katika juhudi za kuwatafuta marubani wake.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.