UTURUKI YAONGEZA ZANA ZA KIVITA KWENYE MPAKA WAKE NA SYRIA


Uturuki imepeleka vifaru vya ziada, magari ya kijeshi na silaha nyingine kwenye mpaka wake na Syria leo Jumamosi baada ya tukio la jeshi lake kuiangusha ndege ya kijeshi ya Urusi lililoongeza joto na mivutano baina ya nchi hizo mbili.

Msafara wa vifaa na zana hizo za kivita kutoka mikoa ya magharibi uliingia katika mkoa wa mpakani wa Gaziantep.

Siku moja kabla, msafara mwingine wa vifaru ulipelekwa kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.

Mapema Jumanne, ndege mbele za Uturuki aina ya F-16 zikiwa katika doria ziliigundua ndege ya kivita iliyokuwa ikiingia katika anga ya Uturuki kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria na baada ya kuionya mara 10 ziliamua kudungua.

Baadae Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitangaza kuwa ndege yake aina ya SU-24 ilikuwa imetunguliwa. Ilianguka katika mkoa wa Syria wa Bayirbucak karibu na wilaya ya Yayladagi ya mkoa wa Hatay kusini mwa Uturuki.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.