BOMU LAUA WATU 20 MSIKITINI

A picture taken on October 23, 2015 in Maiduguri, northeast Nigeria, shows people standing in a mosque following a deadly attack. (Photo by AFP)
Picha iliyopigwa Oktoba 23, 215 mjini Mauduguri, kaskazini mwa Nigeria, ikiwaonesha watu wakiwa wamesimama msikitini baada ya mlipuko wa bomu.Watu ishirini wameuawa na wengine 90 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye msikiti mmoja kaskazini mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa Wakala wa Usimamizi wa Matukio ya Dharura nchini humo (NEMA), mlipuko huo umetokea katika msikiti katika mji mkuu wa jimbo la Borno kaskazini mwa nchi hiyo, siku moja baada ya wapiganaji wa Boko Haram kushambulia eneo la Jiddari Polo kwenye viunga vya mji wa Maiduguri, shambulizi lililosababisha vifo vya watu 15.

Mlipuko huo umetokea katika eneo ambalo siku ya Jumapili jeshi la nchi hiyo lilijibizana risasi na kundi hilo baada ya kupanga kufanya mashambulizi katika mji wa Maiduguri.

"Jana sote tulikimbia baada ya nyumba zetu kushika moto. Asubuhi tumerudi, na wakati tukihesabu idadi ya watu walioungua ndani ya nyumba hizo, bomu lingine likalipuka,” alisema Ibrahim Goni, mkaazi aliyetembelea eneo la mlipuko huo.

Hakuna kundi au mtu ambaye amedai kuhusika na mlipuko huo, lakini mara nyingi maafisa wa Nigeria wamekuwa wakilitupia lawama kundi la Boko Haram kwa matukio hayo, kundi ambalo limekuwa likidaiwa kufanya mashambulizi makali tangu mwaka 2009.

Raisa wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari, amevipa vikosi vya nchi hiyo muda wa hadi mwishoni mwa mwaka huu kuliangamiza kundi hilo.

Uasi wa kundi hilo umeripotwa kupoteza maisha ya watu 20,000 na wengine zaidi ya 2.5 kupoteza makazi tangu mwaka 2009.


The group has expanded its attacks to neighboring African countries including Chad, Niger and Cameroon.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.