DK MAGUFULI KUKUTANA NA WAFANYA BIASHARA


Rais Dk John Magufuli


Rais John Magufuli leo anatarajiwa kukutana na jumuiya ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam katika kile kinachoonekana kama hatua za makusudi za Mkuu huyo wa Nchi kuelezea mipango na matarajio yake kwa sekta binafsi wakati wa utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni.

Japokuwa kikao hicho ni cha kawaida kwenye kalenda ya Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) – ambacho huongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt Magufuli anaonekana kuwa na ujumbe madhubuti wa namna utawala wake unavyotaka kuwa na ushirikiano na sekta binafsi.


Hayo yanafanyika kwa sababu kikao hicho kimekuja chini ya mwezi mmoja tangu alipoapishwa na kabla hajaunda baraza lake la mawaziri.

Aidha, yanafanyika takriban mwezi mmoja tangu mtangulizi wake, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, aongoze kikao kama hicho Oktoba 2.

Taarifa iliyotolewa na katibu mtendaji wa TNBC, Bwana Raymond Mbilinyi, imesema kuwa Rais atatumia mkutano huo kuzunguza na kujadili na wafanyabiashara ili kuwa na diria ya pamoja katika kufikia maendeleo yanayotarajiwa.

Na, iwapo hali itakuwa hivyo, inatarajiwa kuwa Dkt Magufuli atawaasa wafanyabiashara kuchukua hatua za makusudi za kulipa kodi badala ya kufshirikiana na watumishi wasio waaminifu katika kukwepa kodi.

Ijumaa iliyopita, Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, walimsimamisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na maafisa waandamizi watano baada ya kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kiasi cha shilingi bilioni 80 zilizotakiwa kulipwa kodi.

Mpaka sasa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Athumani Diwani, ameripoti kwamba watu wapatao 12 wamekamatwa kuhusiana na skendo hiyo.

Hilo linaonekana kama utekelezaji wa kile ambacho Dk Magufuli alikisema wakati wa hotuba yake ya kulizindua Bunge mjini Dodoma wiki mbili zilizopita alipoashiria kwamba serikali yake haitamvumilia afisa yeyote wa TRA atakayekuwa kikwazo cha serikali kukusanya kodi, hususan kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa.

Wakati wa hotuba yake hiyo, Dk Magufuli aliorodhesha ofisadi kama tatizo la kwanza alililokumbana nalo wakati wa kampeni za uchaguzi.

Alieleza pia kuwa anataka kuona ufisadi, rushwa na urasimu vikizikwa na kuwa historia.

Ni kwa sababu hiyo kwamba Dk Magufuli atatoa onyo kwa watumishi wa umma kuhusu suala la urasimu ambalo limekuwa changamoto kubwa katika ufanyaji biashara nchini kiasi kwamba baadhi ya wawekezaji huamua kwenda nchi nyingine kuwekeza.CHANZO: The Citizen
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.