KIONGOZI MKUU WA WAASI SYRIA AUAWA

Top Syrian rebel leader Zahran Alloush killed in air strike 


Zahran Alloush, mkuu wa kundi la Jaysh al-Islam, ambalo ni miongoni mwa makundi ya waasi yenye nguvu sana katika viunga vya mji wa Damascus vinavyoshikiliwa na waasi, ameuawa katika shambulizi la ndege lililoyalenga makao makuu ya kundi hilo, duru za jeshi la Syria na waasi zimesema.

Duru mbili za waasi zimesema kuwa makao ya siri ya kundi hilo, ambalo ndio kundi kubwa kabisa katika eneo hilo na lenye maelfu ya wapiganaji, yalilengwa na kile walichosema kuwa ni ndege za Urusi.

Jeshi la Syria limesema kuwa Zahran Alloush aliuawa katika shambulio la ndege dhidi ya ngome yake katike eneo la Ghouta ya Mashariki kwenye viunga vya mashariki vya mji mkuu.

Viongozi kadhaa wa makundi ya waasi wameripotiwa kuuawa tangu Urusi ilipoanza mashambulizi makubwa ya anga Septemba 30 katika kumuunga mkono mshirika wake Rais Bashar al-Assad, ambaye vikosi vyake mwaka huu vilionekana kuzidiwa.

Kundi la Jaysh al-Islam, lenye maelfu ya wapiganaji waliopewa mafunzo, ndio kundi kubwa na linaloonekana kujipanga vizuri. Limekuwa likitawala katika eneo la Kusini mwa Ghouta.

Wakati huo huo, kundi hilo limemtangazaAbu Hammam Bowydany kuwa mrithi wa Zahran atakayeliongza kundi hilo. 

Kabla ya kuanzisha kundi la Jaysh al-Islam, Alloush alikuwa ameanzisha kundi la Liwa al-Islam, au Brigedi ya Uislamu, kwa kushirikiana na baba yake Abdallah, anayedaiwa kuishi nchini Saudi Arabia.

Alloush alikuwa katika mgogoro wa kimsingi na makundi ya Dola ya Kiislamu katika Iraq na Sham (ISIS) na al-Qaeda, kwa kuonekana kuwa mtu mwenye nadharia za msimamo wa wastani wa Uislamu.


CHANZO: Today’s zaman na mashirika ya habari.

Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.