MCHUNGAJI AKAMATWA AKIZIKA HIRIZI KANISANI

alt

Polisi katika jimbo la Edo nchini Nogeria wameripotiwa kumtia nguvuni kasisi mmoja wa kanisa la kiinjili mchungaji Ikenna Okafor na wamepanga kumfungulia mashitaka kwa tuhuma za kuzika hirizi katika viwanja vya kanisa lake katika mji wa Benin.

Ingawa kilichozikwa na mtuhumiwa hakijawekwa wazi na polisi, inashukiwa kuwa ni mabaki ya viungo vya mnyama fulani. Matumizi ya hirizi ni jambo la kawaida sana nchini Nigeria, hata makanisani, ambapo taratibu za ibada za kimila huchanganywa na taratibu za kidini na baadhi ya makasisi hutumia hirizi ili kuponya baadhi ya magonjwa.

Katika tukio hili, wakazi wanaoishi jirani na kanisa hilo lililopo katika Mtaa wa Esigie katika mji wa Benin walidai kuwa ilikuwa ni myama fulani aliye hai. Baada ya kumkamata mchungaji Okafor, polisi walimtoa eneo hilo ili kumuepusha asipigwe na wakazi wenye hasira waliovamia viwanja hivyo.

Shuhuda mmoja aitwaye Chinedu Nnamdi, alisema kuwa baba yake alimuamsha saa 8 usiku siku ya Jumamosi kushuhudiwa kilichokuwa kikifanywa na mchungaji huyo. Aliongeza kuwa alimuona mchungaji akizika kitu mbele ya kanisa na baadae kufanya taratibu fulani kwa kulizunguka jengo la kanisa mara kadhaa.

Naibu mrakibu wa Polisi, Osifo Abiodun, ambaye ni msemaji wa jeshi hilo katika jimbo la Edo, amesema kuwa mshukiwa yuko chini ya upelelezi. Alifafanua kuwa mchungaji huyo alitoa maelezo muhimu yatakayosaidia jeshi hilo katika upelelezi wao.


CHANZO: Nigerian Watch
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.