RAIS NKURUNZIZA: TUTAVISHAMBULIA VIKOSI VYA KIGENI

Burundi's President Pierre Nkurunziza
Rais Pierre Nkurunziza wa BurundiRais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, ametishia kupambana na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika vitakavyopelekwa nchini humo, katika maelezo yanayoonekana kuwa yenye utata zaidi tangu kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa nchini mwake.

Mwezi huu, Umoja wa Afrika ulisema kuwa uko tayari kutuma walinda amani 5,000 kwa lengo la kuwalinda raia waliojikuta katika miezi kadhaa za ghasia, jambo lililopelekea kwa mara ya kwanza kwa umoja huo kuingilia kijeshi dhidi ya utashi wa mwanachama wake.

“Kila mtu anapaswa kuheshimu mipaka ya Burundi,” Nkurunziza alisema katika maelezo yake kwenye kituo cha radio cha serikali.

“Iwapo watakiuka misingi hiyo, watakuwa wameishambulia nchi na kila raia wa Burundi atasimama na kupambana nao… nchi itakuwa imeshambuliwa na itajibu mapigo,” alisema katika jibu lake la kwanza la wazi dhidi ya mpango huo wa AU.

Maafisa wengine wa serikali wameshasema kuwa vikosi vyovyote vya walinda amani vitakavyoingia bila idhini ya Burundi vitakuwa vimekwenda kinyume na mamlaka ya nchi hiyo.

Zaidi ya watu 220,000 wameikimbia nchi hiyo tangu mgogro huo ulipolipuka mwezi Aprili kutokana na uamuzi wa Rais Nkurunziza kugombea muhula wa tatu.

Makundi ya upinzani yaliingia barabarani kwa madai kuwa hatua hiyo inakiuka katiba. Lakini alishinda kesi ya kikatiba na hivyo kugombea katika uchaguzi uliofanyika mwezi Julai ambao alishinda.

Mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli, kuendelea kwa ghasia na mashambulizi ya silaha yameibua wasiwasi katika ukanda huu ambao bado una kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 na ambayo vidonda vyake bado havijapona.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.