UN: MATAMSHI YA TRUMP NI HATARI KWA PROGRAMU ZA WAKIMBIZI


Melissa Fleming, spokesperson for the United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR), attends a debate during the 14th World Summit of Nobel Peace Laureates in Rome on December 13, 2014. (AFP photo)
Melissa Fleming, msemaji wa UNHC.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR) limeonya kuwa maneno makali katika kampeni nchini Marekani dhidi ya wakimbizi na Waislamu yanaathiri programu ya nchi hiyo ya makazi kwa ajili ya Wasyria na wakimbizi wengine.

Mtia nia wa kiti cha urais wa chama cha Republican, Donald Trump, jana alitoa wito wa “kuwazuia kabisa” Waislamu kuingia nchini Marekani katika jibu lake dhidi ya mashambulizi yaliyotokea wiki iliyopita katika mji wa San Bernardino, California, ambayo yalisababisha vifo vya watu 14 na kuwajeruhi wengine 21.

Msemaji wa UNHCR, Melissa Fleming, akiongea na vyombo vya habari mjini Geneva amesema kuwa “(Trump) alizungumzia watu wote lakini pia hili linaathiri programu ya wakimbizi.”

“Kwa sababu programu yetu ya wakimbizi haibagui dini,” alisisitiza. “Programu yetu ya makazi inawachagua watu ambazo wana uhitaji mkubwa.”

Marekani imewapa hifadhi wakimbizi wapatao 1,500 pekee kutoka Syria tangu mwaka 2011.

Utawala wa Obama unapanga kuwapokea wakimbizi 10,000 kutoka Syria mwaka huu.

Fleming alielezea wasiwasi wake kuwa magavana wa Marekani wapatao 40 wanapinga mpango huo.

"Tuna wasiwasi kuwa maneno yanayotumika katika kampeni za uchaguzi zinauweka hatarini mpango huu muhumi ambazo unakusudia kuwasaidia watu wenye shida na ambao ni waathirika wa vita ambavyo dunia imeshindwa kuvikomesha," alisema.

Shirika hilo linaitaka Marekani kuwapokea wakimbizi 75,000 kutoka Mashariki ya Kati, Afrika na kwingineko mwaka huu.

Mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump.

Huko nyuma Trump aliwahi kusema kuwa angewafukuza wakimbizi wote wa Syria kama atachaguliwa kuingia Ikulu ya Marekani.

Kampeni za Trump zimekuwa zikigubikwa na maelezo yenye utata dhidi ya wahamiaji, wakimbizi na Waislamu.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.