WASICHANA 2,000 WATOROKA KUKIMBIA UKEKETAJI

Some of the 170 girls who escaped female
Wasichana wapatao 170 waliotoroka kukimbia ukeketaji katika eneo la Magumu katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wakiwa wamekusanyika katika kituo cha Nyumba Salama walikopewa hifadhi kabla ya kuunganishwa na familia zao na kuanza masomo.
Jumla ya wasichana 2,118 wametoroka maskani yao tangu Novemba 15 mwaka huu kukwepa vitendo vya ukeketaji katika maeneo kadhaa ya mkoa wa Mara.

Wasichana hao wamepewa hifadhi katika Kituo cha Uokozi cha Masanga kinachoongozwa na Kanisa Katoliki wilayani Tarime. Baadhi ya wasichana hao wamesema kuwa wanakutana na changamoto ya kukubaliwa na familia zao kwa sababu ya kukimbia vitendo hivyo vya kimila.

Catherine Johannes na Angel Charles walisema kuwa ni wakati sasa kwa jamii kusimama na kuungana pamoja kupinga vitendo hivyo.

“Tunatoa wito kwa serikali na kwa kila mwanajamii kukomesha vitendo hivi. Wasichana wengi hawavifurahii kwa sababu vinatudhalilisha na kuathiri mipango yetu ya baadae,” anasema Catherine.

Katibu wa kituo hicho, Dickson Joseph, aliitaka serikali kuimarisha sheria ili adhabu kali, ikiwemo kifungo cha maisha, itolewe dhidi ya wale wanakandamiza na kudhulumu haki za wasichana.

“Tunahitaji sheria imara na kali ili kukomesha vitendo hivyo vya kikatili,” alisema.

Mamlaka za serikali mkoani Mara na wanaharakati dhidi ya ukiukaji wa haki za wanawake wanatarajia kuanzisha vituo vya uokozi ili kuwaokoa wasichana dhidi ya ukeketaji.

Ukeketaji ni kinyume cha sheria lakini baadhi ya jamii zimeendelea kushikilia utamaduni huo, ambao huwasababishia wasichana udhalilishaji na maumivu makali. Inakadiriwa kuwa mwaka jana, zaidi ya wasichana 1,600 walikeketwa katika vijiji kadhaa vya Wilaya ya Tarime pekee.


CHANZO: The citizen
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.