AMPA SUMU MKEWE NA KUKIMBIA NA KIMADA

 


Bwana mmoja mwenye umri wa miaka 65 katika mkoa wa Aksaray katikati mwa nchi ya Uturuki ameripotiwa kumpa sumu mkewe, akaiba kila kitu katika nyumba na kukimbia na mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikuwa mpangaji wao kwa miezi kadhaa tu.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka mji huo, Zeynel D, baba wa watoto wa nne, ambaye amekuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka 38 alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpangaji wake, ambaye naye ni mke wa mtu na ana watoto wawili.

Mke wa Zeynel D., bibi Cennet D. amedai kuwa wawili hao walipanga kukimbia, na hivyo wakampa sumu, ili waibe dhahabu yenye thamani ya lira 100,000 za Kituruki, kilogramu moja ya lulu, yuro 600 na hati za mali mbalimbali.

Lakini pesa na dhahabu sio vitu pekee walivyoiba na kukimbia. Imeripotiwa kuwa walichukua kila kitu katika nyumba kuanzia vyombo vya ndani, kahawa, chai, maziwa na kadhalika.

Mke anasema kuwa mumewe hakuwa na ajira kwa muda wa miaka 25 hivyo aliinunua nyumba hiyo kwa pesa zake.

"Sikutarajia kitu kama hicho kutoka kwa mwanaume huyo. Amekuwa mume wangu kwa miaka 38 na tuna watoto 4,” alisema bi Cennet D. na kuongeza kuwa hali yake sio nzuri na hawezi kutembea, huku akieleza kuwa mumewe humpigia simu na kutishia kumuua.
Aliendelea kusema kuwa amewasilisha azimio la talaka pamoja na mashitaka katika jeshi la polisi kwa vitisho anavyopewa na mumewe.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.