KAMBI YA KWANZA YA JESHI LA UTURUKI AFRIKA KUFUNGULIWA SOMALIA

First Turkish military base in Africa to open in Somalia 

Uturuki inajiandaa kufungua kambi yake ya kwanza ya kijeshi barani Afrika ambapo maafisa wa kijeshi wa Uturuki watatoa mafunzo kwa askari wa Somalia na vikosi mbalimbali kutoka mataifa mengine ya Afrika kwa lengo la kupambana na kundi la Al-Shabaab, duru za kijeshi zimesema.

Kambi hiyo, ambayo imeidhinishwa na Umoja wa Mataifa, itakuwa kambi ya pili ya jeshi la Uturuki nje ya mipaka ya taifa hili na itawekwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwa mujibu wa makubaliano baina ya serikali za Uturuki na Somalia, zaidi ya vikosi 1,500 vya Kisomali vitapatiwa mafunzo na maafisa 200 wa jeshi la Uturuki.

"Kituo hiki cha mafunzo ya kijeshi kitakuwa kambi muhimu katika kutoa mafunzo ya kejeshi kwa Afrika nzima,” afisa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Uturuki, Emil Tekin, alisema wiki iliyopita.

Afisa hiyo aliongeza kuwa Uturuki pia inapanga kujenga shule ya kijeshi kwa lengo la kutoa mafunzo kwa maafisa wa ngazi za juu na wale wa kawaida.

Uturuki imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi wa Somalia kupitia ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi baina serikali mbili za mataifa hayo kwa miaka mitano sasa.

Aidha, Uturuki iliipatia Somali zaidi ya dola milioni 400 katika kampeni kubwa ya huduma za misaada pindi ilipokuwa ikipambana kulikabili baa la njaa.


Mwezi Desemba, Uturuki ilitangaza kuanzisha kambi yake ya kwanza ya kijeshi nje ya mipaka yake. Kambi hiyo itakayowekwa nchini Qatar imepangwa kuwa sehemu ya makubaliano ya kiulinzi yanayolenga kuzisaidia nchi hizo mbili kukabilia na “adui wa pamoja”.


CHANZO: Daily Sabah
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.