
Watu wawili wameuawa katika tukio la ufyatuaji risasi
karibu na klabu moja ya pombe katikati mwa mji wa Tel Aviv, polisi ya Israeli imesema.
Kwa mujibu wa gazeti la Haaretz, watu wengine watano
wamejeruhiwa katika shambulizi hilo, wawili kati yao wana hali mbaya sana. Wahudumu
wa hospitali wamesema kuwa waliwachukua watu tisa, huku polisi wakisema kuwa
wawili kati yao wamepoteza maisha.
"Vikosi vya polisi vinafanya msako mjini Tel Aviv kuwatafuta
washukiwa walifanya tukio hilo. Majeruhi wote wamepelekwa hospitalini,” msemaji
wa polisi Micky Rosenfeld aliandika kwenye mtandao wa Twitter.
Luba al-Semari, msemaji wa polisi ya Israeli, alisema
katika taarifa kuwa washambuliaji hao wasiojulikana waliondoka eneo hilo baada
ya tukio.
Sababu ya shambulizi hilo mpaka sasa haijajulikana.