Boko harama 89 wahukumiwa kifo Cameroon


Wanachama 89 wa kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamehukumiwa kifo nchini Cameroon baada ya kupatikana na makosa kujihusisha na ugaidi.

Wanachama hao wamehukumiwa na mahakama ya kijeshi kwa mchango wao katika mashambulio kadha eneo la kaskazini mwa Cameroon linalopakana na Nigeria, kwa mujibu wa idhaa ya BBC Hausa.
Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram.

Waliohukumiwa ni sehemu ya wanachama 850 wanaozuiliwa nchini Cameroon kwa kudaiwa kuhusika na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.

Hii ni mara ya kwanza kwa watu kuhukumiwa kifo chini ya sheria mpya za kukabiliana na ugaidi zilizopitishwa mwaka 2014.

Sheria hiyo hupendekeza kifo kwa wanaopatikana na makosa ya ugaidi.
Watu 22 walihukumiwa kifo mwaka 2013.
                                                                 BBC 
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.