NDEGE YA MISRI ILIYOTEKWA YATUA CYPRUS

A crew member of the hijacked aircraft of EgyptAir is seen on the passenger steps after landing at Larnaca airport Tuesday, March 29, 2016. (AP Photo)

Ndege moja ya shirika la ndege la Egypt Air inayofanya safari za ndani kutokea  Alexandria kwenda Cairo imetekwa na kupelekwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus, redio ya serikali imesema.

Shirika la Utangazaji la Cyprus (CBC) limesema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus 320 ilikuwa na watu 55 wakiwemo wafanyakazi saba.

Polisi ya Cyprus ilisema kuwa mtekaji huyo aliwasiliana na chumba cha kuongozea ndege na kuruhusiwa kutua.

Inaripotiwa kuwa mtekaji huyo alimtisha rubani akisema kuwa amevaa mkanda wenye milipuko. Shirika la ndege la Egypt Air limesema kuwa mtekaji aliwaachia watu wote waliokuwa kwenye ndege isipokuwa abiria watatu na wafanyakazi wanne.

Shirika la habari la serikali, MENA, limesema kuwa mtekaji huyo ni raia wa Misri aitwaye Ibrahim Samaha. Alikuwa amekaa kwenye kiti namba K38, imesema bila kutoa maelezo ya kina.

Source: flightradar24.com

Shirika la habari la Cyprus limesma kuwa nchini humo kuna mwanamke aliyekuwa mke wa zamani wa mtu huyo na kwamba anaweza kuwa na sababu binafsi za kufanya tukio hilo.

Mashuhuda wanasema kuwa mtu huyo alirusha barua kwenye aproni ya uwanja wa ndege iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, akitaka ifikishwe kwa mkewe huyo wa zamani kwenye asili ya Cyprus.

Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa na magari ya wagonjwa yametumwa kwenye eneo la tukio.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.