OBAMA: MAREKANI INAUNGA MKONO MAZUNGUMZO YA AMANI NA TALEBAN

US President Barack Obama (R) speaks with Afghanistan President Ashram Ghani during a joint press conference at the White House in Washington, DC, March 24, 2015.  (AFP photo)
Rais Barack Obama (kulia) akizungumza pamoja na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani kwenye mkutano na vyombo vya habari katika ikulu ya Marekani, mjini Washington DC, Machi 24, 2015.


RAIS wa Marekani, Barack Obama, amezungumza na mwenzake wa Afghanistan, Ashraf Ghani kuhusu mazungumzo ya amani na kundi la Taliban, na kueleza uungazi mkono wa Washington kwenye mchakato huo wa maridhiano.

Kauli ya Obama imekuja baada ya maafisa wa Afghanistan, Marekani, Pakistan na China kusema mwezi uliopita kuwa serikali ya Afghanistan na kundi la Taliban walitarajiwa kuwa na mkutano wa moja kwa moja wa mazungumzo ya amani ndani ya wiki ya kwanza ya mwezi Machi katika mji mkuu wa Pakistan.
Wakati akizungumza na Rais Ghani kwa njia ya video, Obama alisisititza juu ya nafasi ya rais huyo wa Afghanistan katika kufanya kazi na majirani wa nchi hiyo ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kusonga mbele katika mchakato wa kufanya maridhiano na kundi la Taliban, taarifa ya Ikulu ya Marekani imesema.

Aidha, Rais Obama alisisitiza uungaji mkono wa Marekani kwenye mazungumzo ya amani yatakayopunguza ghasia na kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo na katika ukanda huo, iliongeza taarifa hiyo.

Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden na Afisa Mtendaji Mkuu Abdullah Abdullah walihudhuria wakati wa mawasiliano hayo.

Ofisi ya Rais wa Afghanistan, imesema kuwa Obama alivipongeza vikosi vya ulinzi vya Afghanistan kwa utendaji mzuri na ujasiri katika kupambana na ugaidi.

“Rais Barack Obama alimweleza Rais Ghani kuwa anavutiwa na utendaji na ujasiri wa vikosi vya ulinzi vya Afghanistan katika kupambana na ugaidi,” ilisema ikulu ya Kabul.

Kwa mujibu wa ripoti moja ya Pentagon iliyotolewa mwezi Januari, hali ya usalama nchini Afghanistan ilizorota katika nusu ya pili ya mwaka 2015, kutokana na wapiganaji wa Kitaliban kufanya mashambulizi zaidi na kusababisha hasara kubwa kwa vikosi vya serikali ya Afghanistan.

Afghanistan imekuwa katika vurugu na ghasia kwa zaidi ya miaka 14 baada ya Marekani na washirika wake kuishambulia nchi hiyo kama sehemu ya vita vya Washington dhidi ya ugaidi. Ingawa mashambulizi hayo ya mwaka 2001 yaliwaondosha madarakani Wataliban, maeneo mengi ya nchi hiyo bado yanakabiliwa na ghasia na ukosefu wa usalama.


Licha ya Rais Obama hapo awali kuahidi kuwa mpaka mwishoni mwa utawala wake atakuwa ameviondosha vikosi vyote vya Marekani, alitangaza mipango ya kubakisha askari 5,500 nchini humo atakapoachia madaraka mwaka 2017.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.