Shein kuzindua baraza la mawaziri Machi 30


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohmaed Shein anatarajiwa kuzindua Baraza jipya la Wawakilishi Machi 30 ikiwa ni hatua za kuelekea  kuanza kazi za Serikali baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.

Akizungumza na wandishi wa habari Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yahaya Khamis Hamad akiongea na waandishi wa habari amesema kwamujibu wa Katiba na taratibu za kuendesha Baraza la Wawakilishi Rais wa Zanzibar ndiye mweye mamlaka ya kuitisha kikao hicho ambapo pia amesema watakitumia kuwaapisha Wajumbe wa Baraza na kuteua Wajumbe watano watakaowakilisha  Baraza ndani ya Bunge.
Mapema Mtendaji huyo wa Baraza alimkabidhi fomu ya kugombea uspika kwa mgombea wa CCM Zubeir Ali Maulid huku akithibitisha kuwa ni mgombea pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo,ambapo akiongea na waandishi mgombea Uspika ambaye  ni wa CCM na ana uhakika wa kupata kiti hicho amesisitiza ahadi zake kuwa Baraza pamoja kuwa ni la CCM halitoyumba na litakuwa na meno.
Baraza hilo la Wawakilishi limekamilika baada ya Uchaguzi Mkuu ambapo Majimbo 54 yamechukuliwa na CCM na viti 22 ni viti maalum vya wanawake huku Mjumbe mwingine na Mwanasheria Mkuu Wazanzibar huku kukiwa kumebakia nafasi10 za upendeleo za Rais  ambapo litafanya baraza hilo kuwa na wajumbe 88 pamoja na spika.
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.