BRAZIL: RAIS ROUSSEFF APOTEZA WASHIRIKA MUHIMU KABLA YA KURA YA KUMNG’OA


Brazil: Rousseff loses key allies ahead of impeach vote

SANTIAGO, Chile

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff, anakabiliwa na shinikizo kubwa la kisiasa baada ya vyama viwili vilivyokuwa washirika katika serikali yake kusema kuwa vitapiga kura ya kutokuwa na imani naye ndani ya bunge.

Muungano wake unaoongozwa na Chama cha Wafanyakazi, umebakiwa na Chama cha Maendeleo chenye wabunge 47 na chama cha Umma chenye wabunge 22.

Rousseff anatuhumiwa kukiuka sheria za bajeti ili kuficha matatizo ya kibajeti kuelekea uchaguzi wa urais  uliofanyika mwaka 2014.

Mchakato huo wa kutengua urais wake unategemea uamuzi wa bunge lenye wabunge 513 ambalo kesho litaanza kujadili iwapo liendelee na mchakato huo au la.

Ili kusonga mbele, kutahitajika theluthi mbili ya kura za wagunge 342 kwa ili hatua hiyo ifikishwe mbele ya bunge la Seneti.

Makamu wa Rais, Michel Temer, ambaye atachukua uongozi wa nchi iwapo bunge la Seneti litapitisha uamuzi wa kutengua madaraka ya rais, amesema kuwa amejiandaa kuchukua uongozi wa nchi iwapo Rousseff atang’olewa.

Kauli ya Temer inakuja siku moja baada ya hotuba yake moja kuvuja mtandaoni ambapo alitangaza hatua kadhaa serikali ya mpito baada ya rais kuondolewa.

Mapema jana Rais Rousseff alisema kuwa ameamua kupambana mpaka dakika ya mwisho kwa ajili ya kuuokoa utawala wake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mawaziri kadhaa wanakiri kuwa upo uwezekano wa kushindwa katika zoezi hilo litakalofanyika Jumapili hii.

“Watu wote wanakubaliana kuwa serikali inakabiliwa na wakati mgumu kabisa kuwahi kuikumba,” limeandika gazeti la Folha de Sao Paulo.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.