UMOJA WA MATAIFA KUTUMA POLISI NCHINI BURUNDI


Representatives from United Nations Security Council (UNSC) members vote during a session. (File photo by AP)
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC)


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloruhusu kutumwa kwa polisi wa Umoja huo nchini Burundi kwa lengo la kusaidia kudhibiti machafuko yanayoendelea nchini humo.

Baraza hilo lenye wanachama 15 jana Ijumaa lilipitisha kwa kauli moja azimio la muswada uliowasilishwa na Ufaransa.

Azimio hilo linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ndani ya siku 15 aandae taratibu za kikosi hicho cha polisi kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika na kwa mashauriano na serikali ya Burundi.

Linatoa fursa ya “kutuma mchango wa polisi ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuongeza uwezo wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia hali ya usalama, kuhamasisha suala la kuheshimu haki za binadamu na kuboresha utawala wa sheria” nchini humo.

Azimio hilo linasisitiza zaidi kuhusu “mkwamo wa kisiasa” nchini Burundi na kuweka mkazo wa hitajio la kuitisha mazungumzo shirikishishi nay a dhati nchini humo.

Burundi iliingia katika mgogoro mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza uamuzi wa kugombea muhula wa tatu, hatua iliyopimgwa na wapinzani kwa hoja kuwa ni kinyume na katiba na inakiuka mkataba wa amani uliosaniwa mjini Arusha mwaka 2006 na kuhitimisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.


Nkurunziza alishinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 70 ya kura milioni 2.8 za uchaguzi uliofanyika mwezi Julai mwaka jana. Hata hivyo, ghasia zilizuka na kunusurika mapinduzi yaliyoshindwa.

Kwa uchache watu 400 wanakadiriwa kuuawa na wengine 250,000 wameikimbia nchi hiyo kutokana na ghasia hizo.

Akizungumzia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, balozi wa Ufaransa kwenye umoja huo, Francois Delattre amesema, “Azimio hili ni hatua ya kwanza katika kuongeza ushiriki wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi kwa lengo la kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinaheshimiwa na kuitaarifu jumuiya ya kimataifa juu ya hali halisi inayoendelea nchini humo.”

Alisema kuwa polisi wapatao 20 mpaka 30 wanatarajiwa kutumwa nchini humo kama “wataalamu na waangalizi” wasiokuwa na silaha.

Balozi wa Burundi kwenye Umoja wa Umoja huo, Albert Shingiro, alielezea utayari wa serikali yake kujadili na kufikia makubaliano juu ya suala hilo, ukubwa na majukumu” ya kikosi hicho.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.