NIGERIA NA CHAD ZAUNGANA KUIKABILI BOKO HARAM

The picture taken on April 3, 2015 shows Nigerien army forces patrolling in pickup trucks near Malam Fatori after the town in northeastern Nigeria was retaken from Boko Haram by troops from Chad and Niger. © AFP
Picha hii iliyopigwa Aprili 3, 2015 inawaonesha askari wa Nigeria wakifanya doria kwenye mji wa Malam Fatori baada ya mji huo ulio kaskazini mashariki mwa Nigeria kukombolewa na vikosi vya Chad na Niger kutoka mikononi mwa waasi wa Boko Haram.Vikosi vya majeshi ya Nigeria na Chad vimeanzisha operesheni ya kijeshi ya pamoja dhidi ya kundi la Boko Haram kwenye mpaka wa mataifa ya Niger na Nigeria.

Brigedia Jenerali Abdou Sidikou Issa, ambaye ni mkuu wa kiufundi wa vikosi vilivyopo katika eneo lenye matatizo la Diffa la Nigeria, amesema kuwa operesheni hizo zinaelenga kukomesha “udhibiti wa maeneo yote” yalinayoshikiliwa na kundi hilo.

“Kazi yetu ni kuhakikisha usalama wa mpaka,” alisema.

Mataifa katika eneo hilo yameunda kikosi cha pamoja chenye mchango mkubwa katika kuisaidia Nigeria kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Mapema mwezi Februari, mataifa manne yanayopakana na Ziwa Chad ambayo ni Niger, Nigeria, Chad na Cameroon – yalianzisha operesheni ya kijeshi ya pamoja kwa kushirikiana na kikosi maalum kutoka Benin, kwa lengo la kukabiliana na kitisho cha wanamgambo wa Boko Haram katika eneo hilo.

Kundi la Boko Haram lilianza harakati zake za uasi mwaka 2009 kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya Nigeria.

Kundi hilo lilipanua mashambulizi yake mpaka kwenye mataifa jirani, hasa o ambao unakadiriwa kugharimu maisha ya watu 17,000 na kuwalazimisha wengine zaidi ya 2.6 kuyakimbia makazi yao.

Wanamgambo hao wamewateka nyara mamia ya vijana, wanawake na watoto katika harakati yao ya miaka sita.

Utekaji wa wasichana wa shule wapatao 200 kutoka mji wa Chibok kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi Aprili mwaka 2014, uliibua hasira ya kimataifa.

Kundi hilo limeungana na kundi la Daesh linalofanya harakati zake za uasi katika nchi za Syria na Iraq.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.