RADI ZAUA 67 NCHINI INDIA

Lightning illuminates the night sky during a storm over the port city of Guwahati, in the northeastern state of Assam, India, on April 18, 2016. (AFP)
Miale ya radi ikiangaza wakati wa dhoruba ya usiku kwenye mji wa badanari wa Guwahati, kaskazini mashariki mwa jimbo la Assam, India, Aprili 18, 2016.Kwa uchache watu 67 wamepoteza maisha yao nchini India kutokana na miale ya radi wakati mvua za msimu zikiikumba nchi hiyo, maafisa wamesema.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Majanga nchini humo (NDMA), mmemetuko wa radi umewaua watu wasiopungua 47, wakiwemo wanawake na watoto, wakati wa dhoruba ya radi iliyopiga usiku mzima katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Bihar Mashariki mwa India na kuwajeruhi wengine 22, hasa katika maeneo ya mashambani.

“Tumethibitisha vifo vya watu 47 na tuna wasiwasi kuwa idadi inaweza kuongezeka kutokana na ripoti mbalimbali kuendelea kumiminika kutoka wilaya nyingine,” amesema Anirudh Kumar, ambaye ni afisa mwandamizi katika wakala wa uratibu wa majanga katika Jimbo la Bihar.

Mashambulizi ya radi hutokea mara kwa mara katika jimbo hilo katika kipindi cha pepo za msimu katika Bahari ya Hindi ambao huanza katika wiki ya pili ya mwezi Juni mpaka mwezi Oktoba. Mvua za masika zilizoanza mapema wiki hii zilikuwa za kwamba za msimu huo.

Wakati huo huo, mamlaka zinasema kuwa katika jimbo jirani la Uttar Pradesh, lililopo maeneo ya kaskazini mwa India, kumeripotiwa vifo vya zaidi ya watu 20 kutokana na mashambulizi ya radi katika kipindi cha siku mbili.

Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za matukio ya Uhalifu, mwaka 2014, zaidi ya watu 2,500 walishambuliwa na radi na kufariki dunia.


Kila mwaka, miale ya radi hugharimu maisha ya maelfu ya watu nchini India, wengi wao wakiwa ni wakulima wanaofanya kazi mashambani.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.