SHAMBULIZI LA KUJITOA MHANGA LAUA 36 MJINI ISTANBUL

36 killed, 147 injured in Brussels-style Istanbul Atatürk Airport terror attacks


Kwa uchache watu 36 wamepoteza maisha na wengine 147 kujeruhiwa katika milipuko ya mabomu ya kujitoa mhanga na shambulizi la silaha za moto katika uwanja mkuu wa ndege wa Istanbul, Atatürk airport, nchini Uturuki.

Baadhi ya safari za ndege zimeanza kurejea katika hali ya kawaida huku baadhi zikifutwa au kuchelewa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gavana wa Istanbul, Vasip Şahin, tathmini inaonesha kuwa washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga walitekeleza mashambulizi hayo katika maeneo matatu tofauti ndani ya uwanja huo.

Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yıldırım, amesema kuwa dalili za awali zinaonesha kuwa kundi la Daesh (IS) lilihusika na shambulizi hilo lakini uchunguzi bado unaendelea.

Afisa mmoja wa afya amesema kuwa majeruhi sita wapo katika hali mbaya.

Milipuko ilitokea kwenye lango la ndege za kimataifa, ndege za ndani, na eneo la maegesho.

Waziri wa Sheria, Bekir Bozdağ, amesema kuwa mmoja wa magaidi aliwafyatulia watu risasi kwa kutumia bunduki aina ya AK-47 na kisha kujilipua.

Rais Recep Tayyip Erdogan ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kuunganisha nguvu katika kupambana na ugaidi, baada ya shambulizi hilo la kigaidi, ambalo ni shambulizi la nne kufanywa mjini Istanbul ndani ya mwaka huu pekee.


Uwanja wa ndege wa Atatürk ni miongoni mwa viwanja vya ndege vyenye safari nyingi zaidi za ndege duniani, ambapo mwaka 2015 uliweza kuwahudumia abiria zaidi ya milioni 60.

(Mzizima 24 WhatsApp: +255 712 566 595)


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.