BADO NAMPENDA, MSITUTENGANISHE

 EMEKA IKE PHOTO/COURTESY

Mwigizaji nyota wa filamu nchini Nigeria, Emeka Ike ameiambia mahakama moja ya mwanzo mjini Lagos kuwa amepeleka ombi mbele ya Mahakama Kuu kuizuia mahakama ya mwanzo isisikilize kesi ya talaka iliyowasilishwa na mkewe waliyefarakana, Emma Ike.

Emma ambaye amekuwa kwenye ndoa na nyota huyo wa Nollywood kwa miaka 16, aliwasilisha ombi la talaka mahakamani mwaka 2015, akidai kuwa mumewe huyo alikuwa akimpiga bila sababu.

Hata hivyo, Ike anakanusha madai hayo na kuiomba mahakama ya Lagos isimtenganishe na Emma.

“Bado ninampenda”, alisema mbele ya mahakama hiyo siku ya Jumanne Julai 12.
Wakili wa Emeka, Abdul Labi-Lawal, aliieleza mahakama hiyo kuwa mteja wake alikuwa amewasilisha mbele ya Mahakama Kuu ombi la kusitisha usikilizaji wa kesi hiyo.

Ombi la Emeka kwenye Mahakama Kuu lililenga kuitaka mahakama hiyo kutamka kuwa mahakama ya mwanzo ya Lagos haina uwezo na uhalali wa kisheria wa kuamua madai hayo ya talaka.

Ombi hilo linasema kuwa ndoa hiyo ilifungwa katika Jimbo la Enugu kwa taratibu za kimila na tamaduni za kabila la Igbo.

Aidha, Emeka aliitaka Mahakama Kuu kutangaza kuwa vikao vyote vilivyofanywa na mahakama ya mwanzo kuhusu ndoa hiyo kuwa ni batili.

Akipinga suala hilo, mwanasheria wa Emma, Iheanyi Awa aliitaka mahakama kutozingatia ombi hilo na badala yake itoe hukumu.


Awa, ambaye alisema kuwa ombi la Emeka lililenga kuzuia hukumu ya mahakama hiyo, aliitarifu mahakama hiyo kwamba si mteja wake wala yeye mwenyewe waliopokea ombi la upande wa mshitakiwa.

WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.