WATU 17 WASHAMBULIWA KWA RISASI NCHINI MAREKANI

Police officers investigate the scene of a mass shooting at Club Blu nightclub in Fort Meyers, Florida, July 25, 2016.
Maofisa wa polisi wakifanya uchunguzi kwenye eneo la tukio la shambulizi la risasi katika ukumbi wa usiku wa Club Blu mjini Fort Meyers, Florida, Julai 25, 2016.

Ufyatuaji wa risasi kwenye ukumbi mmoja wa usiku katika jimbo la Florida nchini Marekani umesababisha kifo cha watu wawili na wengine 15 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Luteni Jim Mulligan kutoka polisi ya kaunti ya Lee,  tukio hilo limetokea usiku kwenye klabu moja ya usiku iitwayo Club Blu katika eneo la Fort Meyers, huko Florida.

Ripoti za awali zilieleza kuwa mmoja wa waathirika wa tukio hilo ni kijana wa miaka 14 huku watoto wengine wenye umri wa miaka 13 wakiwa wamejeruhiwa pia.

Polisi bado hawajathibitisha chanzo cha shambulizi hilo. Vikosi vya usalama na vile vya uokozi vimeelekea katika eneo hilo.

Mshukiwa mmoja amekamatwa kuhusiana na shambulizi hilo lakini haijaieleweka wazi ni washambuliaji wangapi waliohusika na tukio hilo.

Ripoti za mwanzo zinaelezea kutokea kwa mashambulizi mengine mawili jirani na eneo hilo ingawa hayajathibitishwa na duru rasmi.

Mwezi Juni, shambulizi kama hilo kwenye klabu moja ya usiko mjini Orlando, Florida, lilisababisha vifo vya angalau watu 49 na wengine 53 kujeruhiwa.


(Habari zaidi zitawajia kupitia hapa hapa Mzizima 24 …………)

WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.