MAZOEA YAANGAMIZA MAISHA YA KIJANA MWANAMICHEZO

 


Maisha ya kijana Albert (39) yalibadilika moja kwa moja baada ya kupata maradhi ya saratani yaliyosababishwa na steroidi na vinywaji vya kuongeza nguvu ambavyo alikuwa akivitumia ili kupata mwili wenye misuli mikubwa ambao atajivunia mbele ya watu, lakini akapata kitu ambacho hakukitarajia.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Albert alikuwa na mwili mkubwa na misuli maridhawa, akataka kuwa kiigizo kwa vijana wanaotembelea maeneo ya mazoezi (gym), lakini kwa masikitiko makubwa ndoto yake ya kuwa shujaa mwenye mwili mkubwa iliishia kuwa simulizi yenye kuhuzunisha sana. Sasa badala ya kuhamasisha matumizi ya madawa yanayoongeza misuli, akawa mpingaji mkubwa wa madawa hayo.Miaka kadhaa baadaye, Albert alipatwa na saratani ya ini kutokana na maada za kikemikali alizokuwa akizitumia kwa lengo la kukuza misuli na kupunguza baadhi ya maeneo katika mwili wake, kwani ilithibtika kuwa maradhi hayo yalitokana na matumizi hayo yaliyotajwa.


Albert alikuwa na mazoea ya kutumia kalori elfu 10 kwa siku, kiwango ambacho kinachukuliwa kuwa ni kikubwa sana kwa mtu aliyebaleghe, na kwa uchache alikuwa na mazoea ya kunywa kopo 8 za vinywaji vya kuongeza nguvu ili vimsaidie katika ufanyaji wa mazoezi. Lakini Albert amefariki dunia akiwa amekonda kutokana na maradhi ambayo yalimfanya apoteze uzito wote aliokuwa ameupata. 

UNGANA NA MZIZIMA 24:

Kupata habari na matukio kupitia WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.