MILIPUKO YA KUJITOA MHANGA YAUA WATU 80 MJINI BAGHDAD

People gather at the site of a suicide car bomb in the Karrada shopping area, in Baghdad, Iraq, July 3, 2016. (Reuters Photo)
Watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa biashara wa  Karrada mjini Baghdad, nchini Iraq,  Julai 3, 2016. 

Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea katika eneo la soko maarufu mjini Baghdadi nchini Iraq usiku wa kuamkia leo, kituo cha televisheni cha al-Sumaria mimeripoti.

Polisi na maafisa wa afya wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa idadi ya waliofariki dunia inafikia 80.

Kundi la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na mlipuko huo wa kujitoa mhanga lililotokea katika eneo la Karrada kupitia taarifa yake mtandaoni.

Bomu hilo lililopandikizwa kwenye gari lililipuka jirani na mgahawa mmoja katika eneo hilo na kuua watu kadhaa huku wengine 20 wakijeruhiwa.

Video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii imeonesha moto mkubwa kutoka mtaa huo wa Karrada uliotokana na mlipuko huo.

Mlipuko wa pili ulitokea katika eneo la al-Shaab, ambalo lina wakazi wengi wa madhehebu ya Kishia kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq na kusababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa, kituo hicho kimesema.

Mwezi uliopita, vikosi vya Iraq viliwafurusha wanamgambo wa kundi la Daesh kutoka mji wa Falluja uliopo magharibi mwa Baghdad, ambao ulikuwa ngome yao iliyotumika kama kitovu cha uratibu wa mashambulizi hayo.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.