RIPOTI: UNITED WAKUBALIANA NA MATAKWA YA POGBA

1024x534.7096774193549__origin__0x0_Paul_Pogba_Juventus

Vyombo vya habari vya Ufaransa vinaripoti kuwa Manchester United na Juventus hatimaye zimekubaliana kuhudu ada ya uhamisho wa Paul Pogba.

Sakati hilo la muda mrefu linaelekea ukingoni ambapo usiku wa kuamkia leo L’Equipe limeripoti kuwa klabu hizo zimekubaliana kitita cha £92 milioni.

Mwanzo United walikuwa wametoa ofa ya £87milioni pamoja na stahiki nyingine, huku Juve wakishikilia msimamo wao wa kutaka £102 milioni, lakini sasa wamekubaliana kwneye mambo ya msingi.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Pogba atapewa mkataba wa miaka 5 na kwamba United watanunua haki zake za matangazo – na kwamba wakala wa Pogba, Mino Raiola, atapata asilimia 20 ya ada ya uhamisho … £18.4 milioni.


Juve itatumia fedha za uhamisho wa Pogba kumnunua straika wa Napoli, Gonzalo Higuain.

WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.