RONALDINHO: MESSI BADO NI MCHEZAJI BORA DUNIANI

 1022.6666666666666x767__origin__0x0_Lionel_Messi

Kiungo wa zamani kutoka nchini Brazil, Ronaldinho, amesema kuwa mchezaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi bado ni mchezaji bora duniani licha ya kutofainikiwa kushinda kombe katika michuano ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Argentina.

Messi mwenye umri wa miaka 29 alijiuzulu katika timu yake ya taifa mapema mwezi huu baada ya Argentina kushindwa kunyakua kombe la michuano ya Copa America dhidi ya Chile iliyofanyika nchini Marekani.

Mshindi huyo wa mara tano wa Ballon d’Or, aliisaidia timu yake ya taifa kufika fainali nne ikiwemo ile ya Kombe la Dunia la mwaka 2014 dhidi ya Ujerumani, lakini mar azote hakufanikiwa kunyakua kombe licha ya kwamba ndiye mfungaji anayeongoza katika timu ya taifa ya Argentina akiwa na magoli 55 katika michezo 113.

Hivi karibuni nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, aliisaidia Ureno kutwaa taji la michuano ya Mataifa ya Ulaya iliyofanyika nchini Ufaransa na kuibua mjadala wa nani hasa ni mchezaji bora wa dunia kwa sasa, lakini Ronaldinho anamuunga mkono mchezaji mwenzake wa zamani kutoka Barca.

Ronaldinho anasema: “Kwangu mimi, Messi kuacha kushiriki timu ya taifa haibadilishi chochote. Bado anaendelea kuwa mchezaji bora wa dunia. Heshima niliyonayo kwake haijabadilika hata kidogo.


“Na kama kweli ameamua kuacha kushiriki soka la kimataifa basi mchezo huo utamkumbuka, na hata mashabiki zake.”

WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.