TABIA 5 ZA MATAJIRI ZINAZOWASAIDIA KUWA MATAJIRI

richman 


Kwa nini matajiri huzidi kuwa matajiri? Mara nyingi sio kwa sababu ya bahati. Sio kwa sabbau ya familia walizozaliwa. Sio kwa sababu wameshinda bahati nasibu. Matajiri hufanya mambo tofauti na watu wengine.

Miongoni mwa maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni pamoja na sababu za pengo la kipato kuendelea kuongezeka. Katika utafiti wangu, kuna mambo matano ya awali ambayo matajiri hufanya tofauti na watu wengine. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

1.    WANATHUBUTU:

Wanajaribu vitu mbalimbali, wakiwa tayari kwa lolote. Wanafanya uthubutu huo kwa sababu wanajua kwamba kuanguka ni sehemu ya mchakato wa kugundua kipi hasa kitakachofanikisha kujenga himaya kubwa zaidi ya utajiri wao.

2.    WANAJIWEKEZEA:

Matajiri hawaitazami pesa waliyoitumia katika kujistawisha kuwa ni gharama, bali huichukulia kama uwekezaji.

Wanaponunua kitabu, wanapomwajiri mkufunzi, wanapojiunga na makundi ya kunoa bongo zao au kitu kingine kitakachowaongezea maarifa kwa kulipia, huliona hilo kama uwekezaji.


wealthy2

3.    HUSHIRIKIANA NA WALE WANAOTAKA KUWAIGA

Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia: “Ukitaka kuwa tajiri, suhubiana na matajiri”.
Matajiri wanatambua kuwa wanaweza kukuza utajiri wao kwa kushirikiana na wale ambao ni matajiri zaidi yao. Binadamu huchukua tabia na stratejia za wale wanaomzunguka, na matajiri wamejifunza kuitumia fursa hii kuongeza utajiri wao.

4.    MAZOEA YA ASUBUHI:

Matajiri wana utaratibu maalumu ambao hawauachi asilani, utaratibu wanaoufanya kila asubuhi.

Mazoea haya ya asubuhi yanaweza kuwa mazoezi, kupitia malengo yao au kitu chochote kinachowasaidia kuanza siku yao kwa hamasa. Wanaanza siku yao wakiwa imara na kwa hamasa kubwa, ambapo hufanikisha mambo mengi kabla ya mchana kuliko yale yanayofanikishwa na watu wengine ndani ya wiki.5.    UPITIAJI ENDELEVU WA MALENGO YAO:

Matajiri hujiwekea malengo na kisha huendelea kuyapitia malengo hayo mara kwa mara, kufanya mabadiliko na kuongeza mikakati ya kufikia malengo hayo. Mchakato huu wa mrejesho wa haraka huwapa fursa ya kufanya mabadiliko ya haraka kwenye mipango yao ili kuendelea na safari yao kwa kasi kubwa.

Wakati watu wengi hawazingatii sana kuhusu mustakbali wao, matajiri hujikumbusha kile siku kuhusu kule wanakoelekea.


WhatsApp: +255 712 566 595

Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.