SHAMBULIZI LA BOMU LAUA 18 NA KUJERUHI 23 MASHARIKI MWA IRAQ

Iraqi security forces and firefighters stand at the site of a car bomb attack in the town of Khalis, eastern Iraq, on July 25, 2016.
Wanausalama na askari wa kikosi cha kuzima moto wakiwa kwenye eneo lililotokea shambulizi la bomu kwenye mji wa  Khalis, mashariki mwa Iraq, on Julai 25, 2016.

Kwa uchache watu 18 wapoteza maisha na wengine 23 kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa uliotokea katika mji mmoja kwenye jimbo la Diyala nchini Iraq karibu na mpaka na Iran.

Duru za usalama kutoka nchini humo zinasema kuwa shambulizi hilo la bomu limetokea leo asubuhi katika mji wa al-Khalis, kilometa takribani 15 15 (maili 9) kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Baqubah.

Mkuu wa baraza la jimbo, Omar Maan al-Korawi, amesema kuwa gari lililobeba vilipuzi lililipuka karibu na lango la Idara ya Kilimo katika mji huo.

Mpaka sasa, hakuna mtu au kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya shambulizi la bomu kwenye kizuizi cha usalama katika mji wa Kadhimiyah wenye wakazi wengi wa Kishia, kaskazini mwa mji mkuu Baghdad kuua raia wasiopungua 10 na polisi wanne.

Afisa mmoja wa polisi alisema kuwa kwa uchache watu 31 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Takwimu mpya zilizotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq zinaonesha kuwa jumla ya Wairaq 662 waliuawa na wengine 1,457 kujeruhiwa katika vitendo vya kigaidi, ghasia na mgogoro wa kivita katika mwezi wa Juni.

Kwa mujibu wa ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa, idadi ya raia waliokufa ni 382. Ghasia pia ziligharimu maisha ya askari 280 wa vikosi vya usalama ndani ya mwezi huo. Sehemu kubwa ya vifo ilitokea mjini Baghdad, ambapo raia 236 waliuawa.

Maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Iraq yamekumbwa na ghasia tangu kundi la Dola ya Kiislamu kuanza harakati zake nchini humo mwezi Juni mwaka 2014.

Vikosi vya serikali ya Iraq, vikiungwa mkono na wapiganaji wa kujitolea, vimekuwa vikijaribu kuwaondosha wanamgambo hao nchini humo.

WhatsApp: +255 712 566 595


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.