WATURUKI WAISHIO TANZANIA WATAKA SHULE ZA GULEN ZIFUNGWE, WALAANI JARIBIO LA MAPINDUZI

Turks living in Tanzania call for closure of Gülen schools, condemn the coup attempt

Jamii ya Waturuki waishio nchini Tanzania jana walitoa tamko la pamoja kulaani jaribio la mapinduzi lililofanywa na kikundi cha wanajeshi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa mhubiri wa Kiislamu, Fathullah Gulen, huku wakitoa wito wa kufungwa kwa shule zenye uhusiano na mwanazuoni huyo.

Waturuki hao walikusanyika mbele ya ubalozi wa nchini hiyo jijini Dar es Salaam kutoa tamko hilo.


Turks living in Tanzania call for closure of Gülen schools, condemn the coup attempt
“Sisi kama raia na taasisi za Kituruki hapa Tanzania tunalaani vikali jaribio la shambulizi la kijeshi lililofanywa Julai 15 kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali ya Uturuki kwa njia za haramu. Tumefurahi kufahamishwa kuwa jaribio hili limeshindwa na serikali iliyochaguliwa kihalali imeendelea kuhudumu kwa nguvu zote,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

Wakifafanua sababu ya kukusanyika mbele ya ubalozi, watu hao walisema kuwa wanataka kutangaza utii wao na uungaji mkono kwa Rais Recep Tayyip Erdoğan na serikali yake.


Turks living in Tanzania call for closure of Gülen schools, condemn the coup attempt

“Jaribio la mapinduzi ya kijeshi lilifanywa na kikundi kiitwacho FETÖ ambacho kimekuwa kikifanya harakati dhidi ya serikali ya Uturuki kwa muda mrefu. Kwa bahati mbaya, kundi hili pia lina shughuli zake nchini Tanzania kwa jina la Taasisi ya Elimu na Tiba ya Ishik, Shule za Feza na ABITAT (Muungano wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa Viwanda wa Tanzania na Uturuki). Sisi kama jamii na taasisi za Kituruki hatufurahishwi na makundi haya na kwamba wanafanya kazi kwa uhuru katika ardhi ya ndugu zetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” walisema.

“Tunataraji kuwa serikali ya Tanzania itachukua hatua za lazima kukomesha shughuli za kundi hili nchini Tanzania,” walisema, huku wakitoa wito wa wazi kwa serikali kkuzifungia shule zenye uhusiano na kundi hilo.


Turks living in Tanzania call for closure of Gülen schools, condemn the coup attempt


Kundi la Harakati ya Gulen linaloongozwa na mhubiri Fathullah Gulen anayeishi uhamishoni nchini Marekani katika jimbo la Pennsylvania, linatuhumiwa kupanga njama dhidi ya serikali ya Uturuki, kurekodi kwa siri mazungumzo ya maelfu ya watu, wakiwemo maafisa wa serikali. Serikali ya Uturuki imetangaza kuwa kundi hilo ni kitisho kwa usalama wa taifa, na kulitangaza rasmi kuwa ni kundi la kigaidi.


Turks living in Tanzania call for closure of Gülen schools, condemn the coup attempt

Maafisa wa serikali wamekuwa wakieleza mara kwa mara azma yao ya kuendelea kupambana na Harakati ya Gulen kwa njia za kisheria. Wafuasi wa kundi hilo walipenya katika taasisi za dola kwa lengo la kudhibiti mifumo ya dola, kurikodi maafisa na kughushi nyaraka za serikali.


CHANZO: Daily Sabah

Kuapata habari kupitia WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.