WAWILI WAPIGWA RISASI NCHINI MAREKANI

An elderly female patient and a female hospital employee were killed in a shooting in Florida on Sunday. (file photo)

Watu wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi kwenye kituo kimoja cha afya mjini Florida nchini Marekani.

Kwa mujibu wa maafisa wa eneo hilo, tukio hilo limetokea leo saa 8 usiku kwa majira ya nchi hiyo kwenye ghorofa ya tatu ya kituo cha Parrish Medical Center in Titusville.

Mtu aliyekuwa na bunduki alimpiga risasi bibi kizee mmoja aliyekuwa mgonjwa na mhudumu mmoja wa hospitali hiyo.

Polisi wanasema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa, lakini sababu ya kufanya tukio hilo haijajulikana.

Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), bunduki husababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000 nchini humo kila mwaka, idadi ambayo inajumuisha, ajali, mauaji na kujinyonga.


Takwimu zinaonesha kuwa nchini humo kuna kiasi cha bunduki milioni 270 mpaka 300, ambayo ni karibu bunduki moja kwa kila mtu.

(Kupata habari kupitia WhatsApp, ungana nasi kwa: +255 712 566 595)
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.