BOKO HARAM WAPATA KIONGOZI MPYA

This video grab, released on November 9, 2014 shows Abubakar Shekau, who has purportedly been replaced as the leader of the Nigeria-based Boko Haram group. (Via AFP)
Kiongozi wa Boko Haram aliyeenguliwa, Abubakar Shekau.


Kundi la Boko Haram la nchini Nigeria limempata kiongozi mpya. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vyenye uhusiano na kundi hilo, Abu Musab al-Barnawi, ambaye alikuwa msemaji wa kundi hilo, amechukua nafasi ya Abubakar Shekau, ambaye ameliongoza kundi hilo tangu mwaka 2009.

Hata hivyo, sababu za mabadiliko hayo hazijawekwa wazi.

Mapema leo Alhamisi, Shekau alitoa ujumbe wa sauti akisema, “watu wanatakiw akujua kwamba bado tupo,” akionekana kumpinga uamuzi wa kumuondosha kwenye nafasi ya uongozi wake.

Barnawi amedai kuwa kundi lake limeendelea kuwa imara na kwamba mapambano yataendelea dhidi ya nchi za Afrika Magharibi.

“Wanafanya juhudi za kutaka kuifanya jamii kuwa ya Kikristo… wanatumia vibaya hali ya wale walioyakimbia makazi yao kwa sababu ya vita, wanawapa chakula na makazi na kuwabadilisha watoto wao kuwa Wakristo,” alisema akikusudia mataifa ya Afrika Magharibi.

Al-Barnawi alisema kuwa kundi hilo litajibu kitisho hicho kwa kulishambulia kila kanisa watakalolifikia na kuwaua wale (Wakristo) watakaowakuta humo.


Picha ya Maktaba ikiwaonesha wanamgambo wa kundi la Boko Haram

Kundi la Boko Haram lilianza uasi nchini Nigeria mwaka 2009 kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya nchi hiyo. Mpaka sasa watu wapatao 20,000 wameshapoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 2.5 kuyakimbia makazi yao.

Hivi karibuni kundi hilo liliungana na kundi la Dola ya Kiislamu (Daesh) ambalo linafanya harakati zake za uasi katika nchi za Iraq na Syria.


Tukio la mwaka 2014 la kutekwa wasichana 276 lililofanywa na Boko Haram liliifanya dunia kushtuka na kuanza kuwa na itibari juu ya uasi wa kundi hilo.


Boko Haram imeeneza mashambuli yake kutoka kaskazini mashariki mwa Nigeria mpaka katika mataifa jirani ya Chad, Niger na Cameroon.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.