CHADEMA NA JESHI LA POLISI WAONYWA NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

 Screen Shot 2016-08-10 at 5.16.07 PM


Tume ya haki za Binadamu na Utawala bora imelitaka Jeshi la polisi nchini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuacha kutumia lugha zenye viashiria vya uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu badala yake zifanye majadiliano yatakayoleta suluhisho kuhusiana na katazo la maandamano na mikutano ya siasa nchini.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora imefikia uamuzi huo katika mkutano maalum uliotishwa  jijini Dar es salaa na kuwahusisha viongozi mbalimbali akiwemo Msajili wa Vyama Siasa nchini Jaji Francis Mtungi, Katibu mkuu wa Chadema Vincent Mashinji, ingawa waalikwa wengine akiwamo mkuu wa jeshi la polisi, mwanasheria mkuu na chama cha mapinduzi ambao nao kwa mujibu wa tume hiyo walipata mwaliko lakini hawakuhudhiria, huku ikielezwa kuwa IGP na mwanasheria mkuu walitoa hudhuru.

Mwenyekiti wa tume hiyo Bahame Nyanduga amesema nia ya mkutano huo ni kupata suluhu ya kudumu kuhusiana na agizo la lilitolewa na jeshi la polisi June 7 mwaka huu kuhusu kupiga marufuku maandamano na mikutano ya siasa huku CHADEMA ikitangaza kufanya hivyo nchi nzima ifikapo september 1 mwaka huu kupitia operation UKUTA.

Aidha kuhusiana na operesheni “UKUTA” Bw. Nyanduga amekitaka chama hicho kuachana na Neno UDIKTETA kwa kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa misingi demokerasia.


Pia Mwenyekiti Nyanduga ameishauri CHADEMA kuachana na operesheni waliyoita upingaji wa Udikteta Tanzania badala yake wasubiri Tafsiri sahihi itakayotolewa na mahakama kufuatia kufungua shauri hilo katika mahakama kuu kanda ya Dar salaam pamoja na lile la Kanda ya Mwanza.

CHANZO: Channel Ten
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.