GOOGLE YASHUKIWA KWA KUIONDOSHA PALESTINA KWENYE RAMANI ZAKE

google-2


Jukwaa la Wanahabari wa Kipalestina limeishukia Google kwa kufuta jina la Palestina kwenye ramani zake na kuweka jina la Israel.

Katika taarifa yake ya jana, jukwaa hilo lilisema kuwa uamuzi wa Google wa kuiondoa Palestina katika ramani zake ilioufanya tarehe 25 Julai “ni sehemu ya mpango wa Israel wa kuasisi jina lake kama dola halali kwa vizazi vijavyo na kuifuta kabisa Palestina.”

“Hatua hiyo inakusudia kupotosha historia, jiografia na haki ya Wapalestina ya kudai ardhi yao, na ni jaribio haramu la kucheza na akili za Wapalestina, Waarabu na dunia kwa ujmla.”

Jukwaa hilo limesema kuwa hatua hiyo ni “kinyume na mapatano na mikataba yote ya kimataifa”, huku likisisitiza kuwa Google inatakiwa kurudi nyuma kwenye hatua zake hizo.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.