KATIKA PICHA: MAFURIKO MAKUBWA NCHINI YEMEN


Mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua isiyokuwa ya kawaida yamewaua watu 8 katika viunga vya mji wa Sanaa na maeneo mengine kadhaa ya Yemen.

Mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa, kusomba magari na mazao na kuharibu barabara.

Mwanamke akikusanya vitu vyake kutoka kwenye nyumba iliyokumbwa na mafuriko kwenye viunga vya mji wa Sanaa nchini Yemen.

Watoto wakiwa wamepakiwa kwenye gari katika mtaa uliojaa maji mjini Sanaa, nchini Yemen.Wananchi wakikusanya mali zao kutoka kwenye nyumba iliyokumbwa na mafuriko kwenye viunga vya mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Mvua kubwa yaukumba mji wa Sanaa na maeneo mengi ya Yemen huku hali ya hewa ikiwa ya mashaka.

Muonekano wa barabara iliyokumbwa na mafuriko mjini Sanaa, Yemen.Gari na pikipiki zikipita katika barabara iliyokumbwa na mafuriko katika mji wa Sanaa nchini Yemen.

Pikipiki katika mitaa yenye mafuriko mjini Sanaa.

Hali halisi ya mafuriko katika viunga vya mji wa Sanaa.

Wanafamilia wakiwa wamekaa nje ya nyumba iliyoathiriwa na mafuriko mjini Sanaa, Yemen.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.